MBILINYI PHONE AND ELECTRONICS
SASA WAMEKULETEA COMPUTER MPYA NA ZA KISASA
MAFRIJI YA UKWELI, TV BOMBA KUANZIA INCHI 14 HADI 45 SIMU ZA KIJANJA AMBAZO ZINAUWEZO WA KUKAA SIKU 14 BILA KUCHAJIWA, RADIO ZA BAINA MBALIMBALI
OFISI ZETU ZIPO MWANJELWA KARIBU NA STENDI YA MAGARI YAENDAYO TUKUYU.AU TUPIGIE SIMU NO.0764151324
0715151324

SIM

SIM

Tuesday, March 27, 2012

UMOJA wa Waganga Watafiti wa Magonjwa Sugu na Ukimwi kwa Tiba Asilia Tanzania (Umawati) mkoa wa Mbeya, umeelezea mkakati ulionao wa kupambana na magonjwa sugu ili kuhakikisha kuwa serikali inapunguza gharama kubwa za kuagiza dawa za kisasa kutoka nchi za nje; kwamba serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kununua dawa za kupambana na magonjwa sugu na zile za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi wakati utafiti wanaoendelea kuufanya unaweza kusaidia kupunguza kasi ya magonjwa hayo kwa kutumia dawa za asili zinazotokana na miti shamba.
Katibu Mkuu wa Umawati mkoa wa Mbeya, Daniel Mwalukasa, alisema hayo jijini hapa jana alipokuwa akiutambulisha rasmi uongozi wa umoja huo mkoa ili kuweza kuwasaidia wananchi wafahamu kazi na tiba zinazotolewa na waganga wa jadi ambao kwa majukumu yao waliyonayo wamekuwa msaada mkubwa kwa jamii.
Mwalukasa alisema kuwa tiba za jadi zimekuwa zikithaminiwa zaidi kwenye nchi zilizoendelea kuliko matumizi ya dawa za kemikali zinazotokana na madini mbalimbali na kutolea mfano nchi ya China, India na nyinginezo kuwa dawa nyingi zimekuwa zikitengenezwa kisasa kwa mimea ya asili.
Alisema kuwa waganga wa tiba za asili katika mkoa huo wamejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanapata ufumbuzi wa kutosha wa kuwa na dawa sahihi zinazoweza kutibu magonjwa sugu hasa kwa kuzingatia tafiti za kijadi wanazozifanya na jitihada za wataalamu wa tiba za kisasa kuunganisha nguvu zao pamoja.
“Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mkoa uliokuwa na takwimu mbaya kuhusu maambukizi ya ugonjwa hatari wa ukimwi na magonjwa mengine lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda maambukizi yamekuwa yakipungua, kupungua huko kunatokana na uelewa mkubwa wa waganga wa jadi katika kutoa tiba sahihi na wagonjwa wengi wanashuhudia matokeo hayo,” alisema mwenyekiti wa Umawati, Abutwalibu Fungatwende.

No comments:

Post a Comment