MBILINYI PHONE AND ELECTRONICS
SASA WAMEKULETEA COMPUTER MPYA NA ZA KISASA
MAFRIJI YA UKWELI, TV BOMBA KUANZIA INCHI 14 HADI 45 SIMU ZA KIJANJA AMBAZO ZINAUWEZO WA KUKAA SIKU 14 BILA KUCHAJIWA, RADIO ZA BAINA MBALIMBALI
OFISI ZETU ZIPO MWANJELWA KARIBU NA STENDI YA MAGARI YAENDAYO TUKUYU.AU TUPIGIE SIMU NO.0764151324
0715151324

SIM

SIM

Monday, March 5, 2012

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limebariki maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa yaliyopangwa kufanyika kesho majira ya saa 4 asubuhi katika mji wa Iringa. Katika kibali hicho kilichotolewa na jeshi la polisi leo asubuhi kabla ya kutolewa lilikutana na katibu wa IPC Frank Leonard kuomba kufanya marekebisho ya njia na kukubaliana na kuifuta njia ya Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda barabara ya samora na kuishia kanisa la RC mshindo na baada ya hapo kurudi kwa kupita barabara ya Mashine tatu ,Stendi kuu ,M.R Hoteli na kuishia ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. Katika barua hiyo ya jeshi la polisi yenye kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa kwa mtendaji mkuu wa Iringa Press Club yenye kichwa cha Maombi ya kibali cha kufanya maandamano ya amani Imeanza kwa kusema tafadhali rejea barua yako kumb. IPC/02/o12/ Machi 2 ya 03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu. Kibali kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya wanahabari mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4 asubuhi kama ifuatavyo maandamano hayo yataanzia kwenye bustani ya manispaa ya Iringa kuelekea kanisa la Mshindo kwa kupitia barabara ya Uhuru. Baada ya kufika kanisa la Mshindo watapita barabara ya Ubena Club kuelekea stendi kuu ,MR Hotel,Luxury hadi ofisi za mkuu wa mkoa ambapo yataishia . Nakala kwa RPC Iringa kwa taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo Nawatakia maandamano mema Mkuu wa polisi wilaya ya Iringa MOhamed Mkwazu Semunyu Tayari mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ambaye alipaswa kupokea maandamano hayo amekutaka bila kufikia makubaliano na wawakilishi wa wanahabari mkoa wa Iringa katika kikao kilichoanza majira ya saa 6 mchana hadi saa 8 huku mkuu huyo wa mkoa akionyesha kuhofu maandamano hayo kwa madai kuwa ujumbe utakaoandikwa katika mabango unaweza kuchafua hali ya hewa . Wakati huo huo Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepongeza hatua ya chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa(IPC) kutangaza maandamano ya kupinga manyanyaso yanayofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa wao pia wapo pamoja na wanahabari hao kupinga hali hiyo. Katika salamu zake za kupongeza uamuzi huo uliofikiwa na IPC mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Mbeya Bw Christopher Nyanyembe amempongeza mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na viongozi wote wa IPC kwa kuamua kusimama kidete kupinga vitendo vya wanahabari kuendelea kubaguliwa na kunyanyaswa na ofisi ya mkuu huyo wa mkoa na taasisi zake. Kwani amesema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya mikoa hapa nchini kwa ofisi za wakuu wa mikoa kutenga wanahabari na kuwanyanyasa wakati wanapofanya kazi zao. Alisema kuwa iwapo ofisi ya mkuu wa mkoa inatoa mialiko kwa wanahabari kwa ajili ya shughuli zake vikiwemo vikao vya kamati za ushauri za mkoa (RCC) na ziara za viongozi hao wilayani ni wajibu kwa mwanahabari kulipwa kwani hakuna chombo kinachotenga bajeti kwa ajili ya mwanahabari kushiriki viara ya kikazi ya mkuu wa mkoa ama kiongozi mwingine yeyote wakiwemo viongozi hao wa kitaifa. Hivyo alisema kuandamana kwa wanahabari hao mkoa wa Iringa kutawafungua wanahabari wengine kote nchini kuungana na wanahabari mkoa wa Iringa katika kupinga vitendo vya ofisi za wakuu wa mikoa kuendelea kunyanyasa wanahabari. WAKATI wanahabari mkoani Iringa kesho jumanne wamepanga kufanya maandamano ya amani majira ya saa 4 asubuhi kupinga ubaguzi na ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari kufanya kazi yake ,unyanyasaji unaofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa, chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimepanga kukutana na viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) asubuhi ya leo ili kusikiliza madai yao. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza ameomba kukutana na viongozi wa IPC ili kuweza kuyapata kiundani madai hayo na kuangalia kabla ya CCM kufika ofisi ya mkuu wa mkoa kuangalia uwezekano wa kumaliza tofauti hizo. Kwani alisema CCM haiungi mkono suala la vyombo vya habari kutengwa ama kunyanyaswa wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi na kuwa CCM na jamii inategemea vyombo vya habari kupata taarifa mbali mbali. Kiponza alisema kusudi la kukutana na viongozi hao wa wanahabari katika ofisi yao leo si kwa ajili ya kuzuia maandamano hayo bali ni kwa ajili ya kusikiliza madai yao na kuwa suala la wanahabari kudai haki yao ni wajibu wao ambao wao kama chama hawawezi kuingilia kati . Mbali ya mwenyekiti huyo mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM pia ameeleza kusikitishwa na vyombo vya habari mkoani Iringa kuendelea kunyanyasika na kubaguliwa wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na kuwa kwa upande wake hakupendezwa na manyanyaso waliyofanyiwa wanahabari hao wakati wa ziara ya makamu wa Rais na kuwa alimwagiza katika wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha kukutana na wanahabari hao . Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya uongozi wa mkoa kuwalaza nje wanahabari hao wakati wa ziara ya Rais Kikwete wilaya ya Njombe na ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghirib Bilala aliyefanya ziara yake katika wilaya ya Makete ,Njombe ,Mufindi na Iringa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment