MBILINYI PHONE AND ELECTRONICS
SASA WAMEKULETEA COMPUTER MPYA NA ZA KISASA
MAFRIJI YA UKWELI, TV BOMBA KUANZIA INCHI 14 HADI 45 SIMU ZA KIJANJA AMBAZO ZINAUWEZO WA KUKAA SIKU 14 BILA KUCHAJIWA, RADIO ZA BAINA MBALIMBALI
OFISI ZETU ZIPO MWANJELWA KARIBU NA STENDI YA MAGARI YAENDAYO TUKUYU.AU TUPIGIE SIMU NO.0764151324
0715151324

SIM

SIM

Tuesday, March 27, 2012

UMOJA wa Waganga Watafiti wa Magonjwa Sugu na Ukimwi kwa Tiba Asilia Tanzania (Umawati) mkoa wa Mbeya, umeelezea mkakati ulionao wa kupambana na magonjwa sugu ili kuhakikisha kuwa serikali inapunguza gharama kubwa za kuagiza dawa za kisasa kutoka nchi za nje; kwamba serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kununua dawa za kupambana na magonjwa sugu na zile za kupunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi wakati utafiti wanaoendelea kuufanya unaweza kusaidia kupunguza kasi ya magonjwa hayo kwa kutumia dawa za asili zinazotokana na miti shamba.
Katibu Mkuu wa Umawati mkoa wa Mbeya, Daniel Mwalukasa, alisema hayo jijini hapa jana alipokuwa akiutambulisha rasmi uongozi wa umoja huo mkoa ili kuweza kuwasaidia wananchi wafahamu kazi na tiba zinazotolewa na waganga wa jadi ambao kwa majukumu yao waliyonayo wamekuwa msaada mkubwa kwa jamii.
Mwalukasa alisema kuwa tiba za jadi zimekuwa zikithaminiwa zaidi kwenye nchi zilizoendelea kuliko matumizi ya dawa za kemikali zinazotokana na madini mbalimbali na kutolea mfano nchi ya China, India na nyinginezo kuwa dawa nyingi zimekuwa zikitengenezwa kisasa kwa mimea ya asili.
Alisema kuwa waganga wa tiba za asili katika mkoa huo wamejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanapata ufumbuzi wa kutosha wa kuwa na dawa sahihi zinazoweza kutibu magonjwa sugu hasa kwa kuzingatia tafiti za kijadi wanazozifanya na jitihada za wataalamu wa tiba za kisasa kuunganisha nguvu zao pamoja.
“Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mkoa uliokuwa na takwimu mbaya kuhusu maambukizi ya ugonjwa hatari wa ukimwi na magonjwa mengine lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda maambukizi yamekuwa yakipungua, kupungua huko kunatokana na uelewa mkubwa wa waganga wa jadi katika kutoa tiba sahihi na wagonjwa wengi wanashuhudia matokeo hayo,” alisema mwenyekiti wa Umawati, Abutwalibu Fungatwende.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ametangaza kuwa Aprili mosi ni siku ya mkesha wa kulinda kura kwa kila mwananchi mpenda demokrasia na maendeleo katika jimbo hilo. Akihutubia mikutano ya kumnadi mgombea wa chama hicho, Joshua Nassari, katika maeneo mbalimbali ya kata za Songoro, Ngarenanyuki, Leguruki, Nkoanrua na Maji ya Chai, Mbowe aliwataka wananchi wote wa jimbo hilo, hususan vijana, kukusanyika makao makuu ya Halmashauri ya Meru, ambako majumuisho ya mwisho ya kura yatafanyika kabla ya kutangaza matokeo. “Ndugu zangu wana wa Arumeru Mashariki Aprili moja ambayo ni siku ya kupiga kura tumetangaza kuwa ni mkesha wa kulinda kura pale Halmashauri Usa River, wananchi wote, hasa vijana mkishapinga kura siku hiyo kwa amani kabisa, kwa utulivu, bila kumpiga wala kumsukuma mtu yeyote sindikizeni masanduku ya kura mpaka Usa River, tukifika pale tutasubiri matokeo pamoja ikibidi hata kukesha lakini hatutaondoka mpaka tumepata matokeo. Mbowe alisema kuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa kuwa Chama cha Mapinduzi na serikali yake wana mbinu nyingi za kuiba kura. Akiwa katika kijiji cha Maruango, kata ya Leguruki, alisema kuwa uchaguzi wa Arumeru Mashariki si uwanja wa vita, akisisitiza kauli aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho Machi 9, mwaka huu, kuwa CHADEMA itafanya mikutano ya amani na kistaarabu bila kumtukana mtu yeyote, huku akilitaka Jeshi la Polisi kuwa uwepo wake Arumeru kuwe ni sehemu ya matumaini na haki kutendeka, si kuibeba CCM na kuwatia hofu na woga wananchi. Aliongeza kuwa utawala wa CCM umekuwa ukiwatisha watu badala ya kuwa sehemu ya matumaini na haki za wananchi, akionya kuwa hakuna utawala wa kidhalimu uliowahi kudumu milele, kwani CCM sasa badala ya kuwatia moyo wananchi na kuwapatia haki wamegeuka kuwatia hofu na kuwatisha, ikiwa ni ishara ya utawala wa kidhalimu. “Ndugu zangu polisi ambao pamoja na kutupiga mabomu bado tunawatetea, nawaombeni sana muwe sehemu ya haki na matumaini ya wananchi hawa, fanyeni kazi yenu ya kulinda amani na usalama wa raia na mali zao, msifanye kazi ya kuibeba CCM, wala nguvu zenu hizo za kuibeba CCM hazitasaidia, uwepo wenu hapa usiwe kuwalinda mafisadi bali kulinda haki na matumaini ya watu hawa. “CCM wanafanya vitendo vya kihalifu kwa watu wanaowapinga kifikra, kama hivi vya kumpiga mzee wa miaka sabini, wanapiga raia, tunataka polisi waliomwagwa hapa kwa wingi wachukue hatua dhidi ya wavunja sheria hao. Aliongeza kuwa chama tawala kimeleta wabunge 50 na serikali imekwenda likizo kwa vile mawaziri wamehamia hapa huku Waziri wa Uratibu na Mahusiano, Stephen Wassira, akiongoza kampeni za matusi badala ya kutengeneza mahusiano. “Mary Nagu naye anakuja hapa anatisha wajasiriamali kuwa wananchi wasipoichagua CCM watakiona, huyu ana pesa za wapi, serikali haina pesa zake, fedha zote ni mali ya umma. Kila Mtanzania anao uhuru na haki ya kujiunga na chama chochote anachokitaka. Tunasema hivi sisi tutawakosoa na kuwapinga kwa ajili ya maslahi ya wananchi,” alisema Mbowe. Mzee wa CHADEMA apigwa na kijana wa CCM Mzee mwenye umri wa miaka 65, Eliya Samweli, amedai kupigwa na kijana aliyemtaja kwa jina la Elibariki Karelia, kwa sababu ya uamuzi wake wa kujiunga na CHADEMA hivi karibuni na kukabidhiwa kadi ya chama hicho wiki iliyopita. Akizungumza katika mkutano wa kampeni mbele ya Mbowe, Mzee Samweli alisema kuwa kijana huyo alimkuta akinywa soda madukani Maruango, akamtisha na kumnyang’anya simu na baadaye saa tatu kumvamia nyumbani kwake na kuanza kumpiga. Alisema watoto wake walipiga yowe kuomba msaada wa majirani, ambapo mtuhumiwa alikimbia, huku akimtishia kuwa angemchomea moto nyumba yake. CCM yamwaga matusi Katika hali isiyo ya kawaida mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Sioi Sumari ulitawaliwa na maneno ya matusi na vijembe dhidi ya viongozi wa CHADEMA. Hali hiyo ilijitokeza jana wakati mgombea wa CCM , Sioi Sumari, alipokuwa akihutubia jukwaani aliporwa kipaza sauti na Meneja wa Kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, ambaye alianza kumshambulia Katibu Mkuu wa CHADEMA , Dk. Willibrod Slaa kwa matusi akimwita kichaa. Hatua hiyo ilitokana na kitendo cha helikopta ya CHADEMA kupita juu kwa mbali na ulipokuwa ukifanyika mkutano wa CCM, na kusababisha wananchi wengi waliokuwa kwenye mkutano huo kushangilia kwa kutumia salamu ya CHADEMA ya “Peoples Power” huku wakionyesha vidole viwili juu. Hata hivyo ilibainika baadaye kuwa waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , mgombea wa CHADEMA, Nassari, na kiongozi wa kampeni hizo Vicent Nyerere ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wao wa mwisho eneo la Maji ya Chai. Naye mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani aliwalalamikia makada wa CHADEMA kwa kumsakama kuwa ni mganga wa kienyeji wakati yeye ni muumini mzuri wa Kanisa la Anglikana. NEC yawakoroga wapiga kura UAMUZI wa Tume ya Uchaguzi wa kutaka kutuma taarifa za vituo vya kupigia kura kwa njia ya simu katika uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki umewakoroga baadhi ya wananchi, huku wengine wakiunga mkono. NEC juzi ilisema kuwa sasa itawajulishwa wananchi vituo vyao vya kupigia kura kwa njia ya simu, jambo ambalo limezua zogo kwa baadhi ya maeneo. Wakiongea kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wananchi wamekubaliana na utaratibu huo wakisema utawarahisishia na utawaondolea usumbufu usio na lazima wa kwenda kusimama muda mrefu kwenye vituo kutafuta majina yao. “Utaratibu huu ni mzuri kwa sababu utatupunguzia usumbufu wa kwenda kusimama muda mrefu kwenye vituo vya kupigia kura tukitafuta majina,” alisema Jerome Kitomari. Hata hivyo, wanaoupinga walisema kuna hatari ya kusababisha wapigakura wengi kukosa fursa ya kupiga kura pale itakapotokea mtu akapata maelekezo ya kituo lakini siku ya kupiga kura jina lake likakosekana. “Huu utaratibu unaweza kuwa ‘changa la macho’ kwani tunaweza kutumiwa majina ya vituo kwenye simu lakini tukifika pale tukaambiwa majina hayaonekani kwenye orodha kwa siku hiyo sidhani kama itakuwa rahisi kupata msaada wa kujua jina lako liko kituo kipi hivyo ni dhahiri hautapiga kura,” alisema Salome Pallangyo. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa alisema kuwa utaratibu huo ni mzuri kama ukitekelezwa ipasavyo lakini alitilia shaka kwa kile alichoeleza kuwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ulitangazwa kuwa ungetumika lakini ulishindikana. Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasias Kagenzi, mwishoni mwa wiki aliviandikia barua vyama nane vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni hapa akiwataka wawaelimishe wapiga kura namna ya kutumia ya simu za kiganjani kujua kituo cha kupiga kura . Kwenye barua hiyo yenye kumbukumbu namba E . 50/9/2012/40 ya machi 24 , mwaka huu, Kagenzi alieleza kuwa kila mpiga kura atatakiwa kuandika namba yake kwenye kitambulisho chake kisha ataituma kwenda namba 15540 ambapo atatumiwa taarifa yake pamoja na kituo atakachotakiwa kupigia kura.

Monday, March 5, 2012

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limebariki maandamano ya wanahabari mkoa wa Iringa yaliyopangwa kufanyika kesho majira ya saa 4 asubuhi katika mji wa Iringa. Katika kibali hicho kilichotolewa na jeshi la polisi leo asubuhi kabla ya kutolewa lilikutana na katibu wa IPC Frank Leonard kuomba kufanya marekebisho ya njia na kukubaliana na kuifuta njia ya Uhindini na badala yake kuruhusu maandamano hayo kutumia barabara ya Uhuru kutoka Bustani ya Manispaa ya Iringa kwenda barabara ya samora na kuishia kanisa la RC mshindo na baada ya hapo kurudi kwa kupita barabara ya Mashine tatu ,Stendi kuu ,M.R Hoteli na kuishia ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. Katika barua hiyo ya jeshi la polisi yenye kumbukumbu namba IRI/A./14/VOl.x11/178 iliyotumwa kwa mtendaji mkuu wa Iringa Press Club yenye kichwa cha Maombi ya kibali cha kufanya maandamano ya amani Imeanza kwa kusema tafadhali rejea barua yako kumb. IPC/02/o12/ Machi 2 ya 03/03/2012 inayohusu kichwa cha habari hapo juu. Kibali kimetolewa cha kufanya maandamano ya amani kwa Klabu ya wanahabari mkoa wa Iringa mnamo tarehe 6/3/2012 muda wa saa 4 asubuhi kama ifuatavyo maandamano hayo yataanzia kwenye bustani ya manispaa ya Iringa kuelekea kanisa la Mshindo kwa kupitia barabara ya Uhuru. Baada ya kufika kanisa la Mshindo watapita barabara ya Ubena Club kuelekea stendi kuu ,MR Hotel,Luxury hadi ofisi za mkuu wa mkoa ambapo yataishia . Nakala kwa RPC Iringa kwa taarifa na RTO tafadhali panga askari wa kuongoza maandamano hayo Nawatakia maandamano mema Mkuu wa polisi wilaya ya Iringa MOhamed Mkwazu Semunyu Tayari mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ambaye alipaswa kupokea maandamano hayo amekutaka bila kufikia makubaliano na wawakilishi wa wanahabari mkoa wa Iringa katika kikao kilichoanza majira ya saa 6 mchana hadi saa 8 huku mkuu huyo wa mkoa akionyesha kuhofu maandamano hayo kwa madai kuwa ujumbe utakaoandikwa katika mabango unaweza kuchafua hali ya hewa . Wakati huo huo Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mbeya (MBPC) kimepongeza hatua ya chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa(IPC) kutangaza maandamano ya kupinga manyanyaso yanayofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa wao pia wapo pamoja na wanahabari hao kupinga hali hiyo. Katika salamu zake za kupongeza uamuzi huo uliofikiwa na IPC mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Mbeya Bw Christopher Nyanyembe amempongeza mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na viongozi wote wa IPC kwa kuamua kusimama kidete kupinga vitendo vya wanahabari kuendelea kubaguliwa na kunyanyaswa na ofisi ya mkuu huyo wa mkoa na taasisi zake. Kwani amesema kuwa kumekuwepo na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya mikoa hapa nchini kwa ofisi za wakuu wa mikoa kutenga wanahabari na kuwanyanyasa wakati wanapofanya kazi zao. Alisema kuwa iwapo ofisi ya mkuu wa mkoa inatoa mialiko kwa wanahabari kwa ajili ya shughuli zake vikiwemo vikao vya kamati za ushauri za mkoa (RCC) na ziara za viongozi hao wilayani ni wajibu kwa mwanahabari kulipwa kwani hakuna chombo kinachotenga bajeti kwa ajili ya mwanahabari kushiriki viara ya kikazi ya mkuu wa mkoa ama kiongozi mwingine yeyote wakiwemo viongozi hao wa kitaifa. Hivyo alisema kuandamana kwa wanahabari hao mkoa wa Iringa kutawafungua wanahabari wengine kote nchini kuungana na wanahabari mkoa wa Iringa katika kupinga vitendo vya ofisi za wakuu wa mikoa kuendelea kunyanyasa wanahabari. WAKATI wanahabari mkoani Iringa kesho jumanne wamepanga kufanya maandamano ya amani majira ya saa 4 asubuhi kupinga ubaguzi na ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari kufanya kazi yake ,unyanyasaji unaofanywa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa, chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimepanga kukutana na viongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) asubuhi ya leo ili kusikiliza madai yao. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza ameomba kukutana na viongozi wa IPC ili kuweza kuyapata kiundani madai hayo na kuangalia kabla ya CCM kufika ofisi ya mkuu wa mkoa kuangalia uwezekano wa kumaliza tofauti hizo. Kwani alisema CCM haiungi mkono suala la vyombo vya habari kutengwa ama kunyanyaswa wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi na kuwa CCM na jamii inategemea vyombo vya habari kupata taarifa mbali mbali. Kiponza alisema kusudi la kukutana na viongozi hao wa wanahabari katika ofisi yao leo si kwa ajili ya kuzuia maandamano hayo bali ni kwa ajili ya kusikiliza madai yao na kuwa suala la wanahabari kudai haki yao ni wajibu wao ambao wao kama chama hawawezi kuingilia kati . Mbali ya mwenyekiti huyo mbunge wa jimbo la Kilolo Prof.Peter Msolla ambaye ni mjumbe wa NEC ya CCM pia ameeleza kusikitishwa na vyombo vya habari mkoani Iringa kuendelea kunyanyasika na kubaguliwa wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa na kuwa kwa upande wake hakupendezwa na manyanyaso waliyofanyiwa wanahabari hao wakati wa ziara ya makamu wa Rais na kuwa alimwagiza katika wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha kukutana na wanahabari hao . Hatua hiyo imekuja baada ya baada ya uongozi wa mkoa kuwalaza nje wanahabari hao wakati wa ziara ya Rais Kikwete wilaya ya Njombe na ziara ya Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghirib Bilala aliyefanya ziara yake katika wilaya ya Makete ,Njombe ,Mufindi na Iringa hivi karibuni.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeendelea kujisiriba matope kwa kuendesha mauaji ya kiholela kwa raia ambapo jana askari wa jeshi hilo wamemuua mwanafunzi Said Msabaha wa shule ya Sekondari Lupa iliyopo wilayani Chunya mkoani hapa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupa wilayani humo William Patrick Mbawala, ameuambia mtandao wa huu kuwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chake alikamatwa na askari hao akiwa na wenzake watatu kwa tuhuma za wizi wa simu Februari 29, mwaka huu na baadaye waliachiwa kwa dhamana. Amesema baada ya kutolewa katika kituo kidogo cha Lupa, Marehemu alionekana kuwa hali yake imedhoofika na alipoulizwa alieleza kuwa alipokuwa kituoni hapo alipigwa na askari polisi jambo ambalo liliwalazimu kumpeleka katika zahanati ya kijiji hicho chini ya Mganga aliyemtaja kwa jina la Dr. Solomon. Amesema Baada ya kuona hali yake inaendelea kuwa mbaya ndipo lilipochukuliwa jukumu la kumpeleka Hospitali ya wilaya na bahati mbaya akafia njiani hata kabla ya kumfikisha katika Hospitali hiyo. Naye Baba mzazi wa marehemu, Msabaha Hussein, amesema kuwa baada ya kufariki mtoto wake akachukua jukumu la kupeleka maiti kituo cha polisi ili wahusike katika kuuzika mwili wa marehemu kwa kile aichodai kuwa kifo cha mwanae ni matokeo ya kipigo walichokitoa alipokuwa mikononi mwao. Nao baadhi ya wananchi waliohojiwa kwa masharti ya kuhifadhi majina yao wamesema kuwa baada ya kuona hali hiyo na kwasababu askari wanaodaiwa kuhusika wanawafahamu ndipo walipochukua jukumu la kuwatafuta askari hao ambao tayari walikuwa wametokomea kusikojulikana. Wamesema kuwa baada ya kuwakosa katika makazi yao, waliamua kuzichoma moto nyumba za askari hao ambao ni Copl. Maxmillian, PC Mjuni na PC Hery ambapo hawakuishia hapo walimtafuta PC Fadhil bila mafanikio na kuharibu samani zake za ndani huku wakishinikiza Jeshi la polisi kuuzika mwili wa marehemu huyo. Afisa upepelezi wa Jeshi hilo mkoani Mbeya (RCO) Elias Mwita alipotakiwa kuzungumzia sakata hilo alisema kuwa ni mapema mno. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Chunya Deodatus Kinawiro ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo alipotafutwa ili aweze kuzungumzia tukio hilo hajaweza kupatikana kupitia simu yake ya kiganjani. Awali askari hao walidaiwa kutorokea Jijini Mbeya lakini taarifa kutoka ndani ya vyanzo vya kikosi kazi cha mtandao huu jeshi la Polisi mkoani Mbeya vimesema kuwa askari hao walikuwa bado hawajakamatwa wala kuonekana katika viunga vya Jiji la Mbeya. Tukio hilo la kinyama limetokea siku chache baada ya askari wa jeshi hilo PC Maduhu kuhusika kumuua aliyekuwa Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TEKU kilichopo jijini mbeya Daniel Godluck Mwakyusa (31) February 14, mwaka huu.
chanzo cha habari na.ezekiel kamanga